Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Soko kuu la Alhamisi la kaunti ya Isiolo lafunguliwa

Soko kuu la Alhamisi la kaunti ya Isiolo lafunguliwa

Wiki moja tu baada ya manispaa ya kaunti ya Isiolo kulifunga soko la alhamisi mwenyekiti wa manispaa ya Isiolo Osman Halakhe ametangaza kufunguliwa kwa soko hilo na kusema kuwa wafanyabiashara wa kaunti ya Isiolo na wale wa kutoka kaunti za nje wana uhuru wa kulitumia.

Kufungwa kwa soko hilo kulipelekea wafanyakazi na wanabiashara  wakiongozwa na mwenyekiti wa vijana katika soko hilo kueleza malalamishi yao. Wafanyakazi hao walisema kuwa soko hilo ndilo liliwapa vijana ajira na kupunguza visa vya ukosefu wa usalama, na vilevile matumizi ya mihadarati.

Osman amesema kuwa kufunguliwa kwa soko hilo kutasaidia kurejesha biashara ya mitumba ambayo ndiyo kitega uchumi kwa wafanyabiashara wengi. Aidha Osman amesema kuwa kufungwa kwa soko hilo haikuwa njia ya kuwafukuza wafanyabiashara kutoka kaunti ya meru.

Mwaka jana afisi inayokagua Viwango vya bidhaa humu nchini iliondoa marufuku  ya nguo za mitumba iliyokuwa imewekwa na serikali  baada ya wafanyabiashara wa nguo hizo kulalamikia hali ngumu ya maisha.
RELATED ARTICLES

Makadirio ya uzalishaji wa chakula katika sekta ya Ukulima

Mazao ya vyakula yanatarajiwa kuongezeka kati ya mwaka wa 2018 hadi 2022 Ongezeko hili linatarajiwa   kufuatia vijana katika kaunti...

Sen. Abshiro aitaka serikali ya Isiolo kuzisaidia hifadhi za jamii.

Seneta mteule Halake Abshiro, ameitaka serikali ya kaunti ya Isiolo kutenga fedha Zaidi  katika bajeti yake kwa manufaa ya wakaazi wanaoishi katika...

NYOTA YA MATUMAINI KWA VIJANA WANAOITAJI KUJIKIMU NA KOZI ZA KIUFUNDI

Huku Kenya ikizidi kufanikisha ruwaza ya mwaka wa elfu mbili na thelathini, vijana wanazidi kutakiwa kujikimu na ujuzi wa kiteknikali ili waweze...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Makadirio ya uzalishaji wa chakula katika sekta ya Ukulima

Mazao ya vyakula yanatarajiwa kuongezeka kati ya mwaka wa 2018 hadi 2022 Ongezeko hili linatarajiwa   kufuatia vijana katika kaunti...

Sen. Abshiro aitaka serikali ya Isiolo kuzisaidia hifadhi za jamii.

Seneta mteule Halake Abshiro, ameitaka serikali ya kaunti ya Isiolo kutenga fedha Zaidi  katika bajeti yake kwa manufaa ya wakaazi wanaoishi katika...

NYOTA YA MATUMAINI KWA VIJANA WANAOITAJI KUJIKIMU NA KOZI ZA KIUFUNDI

Huku Kenya ikizidi kufanikisha ruwaza ya mwaka wa elfu mbili na thelathini, vijana wanazidi kutakiwa kujikimu na ujuzi wa kiteknikali ili waweze...

Makadirio ya mapato ya Kaunti ya Isiolo.

Mapato ya Kaunti ya Isiolo yanatarajiwa kuongezeka kati ya 2017-2022.  Ongezeko hili linatarajiwa kuwa thabiti. Mwaka wa 2017/18...