Staff Mail

CATHOLIC DIOCESE OF ISIOLO COMMUNICATION DEPARTMENT

GIZA TOTORO KATIKA ENEO LA POOLSMAN KAUNTI YA ISIOLO BAADA YA TAA KUZIMA WIKI TATU

Huku wanabiashara wadogo wadogo wakipitia hali ngumu ya uchumi kutokana na mkurupuko wa janga la corona,wanaofanyia eneo la Pools Man Kulamawe wadi ya Bulapesa wanaeleza chumvi iliyotiwa katika kidonda chao baada ya taa za eneo hilo kuzima takriban wiki tatu zilizopita. Wakizungumza na radio shahidi wameonyesha gadhabu na kutishia kufanya maandamano iwapo hakutakua na suluhu la kudumu. Sio mara ya kwanza wanabiashara wa Poolsman kushuhudia giza totoro,bali ni jambo wanaloeleza kuwa hutokea baada ya mda. Wameshuhudia visa vya wizi kutokana na giza lilo eneo hilo hivyo wanaofia hata masiha yao. Wameeleza kwamba masaa yalioongezwa ya kafyu hayawasaidii kwani wateja hawaji kwa hofu ya kuvamiwa na wezi.Wametaka serikali ya kaunti ya Isiolo kuingilia kati na kutatua suala hilo. Juhudi zetu kuzungumza na msimamizi wa manispaa Osman Halake zimefua dafu ambapo amesema kwamba ni matatizo yasiyo epukika na tayari mwanakandarasi anashughulikia suala hilo . Pia ameahidi kuwa takriban wiki mbili zijazo atakuwa amerekebisha. NA BETTY LUKE KATHAMBI