Staff Mail

CATHOLIC DIOCESE OF ISIOLO COMMUNICATION DEPARTMENT

VERY REV. FR. JOSEPH MWONGELA AMETEULIWA KAMA ASKOFU JIMBO KATOLIKI LA KITUI

NA BETTY LUKE...Baba mtakatifu Francisco amemteua Rev. Fr. Joseph Mwongela kuwa askofu wa nne wa jimbo katoliki la Kitui. Taarifa ya kuteuliwa kwa Askofu Joseph Mwongela zilitangazwa rasmi Jana 17th Mechi katika mji Roma kisha barua ya kuteuliwa kwake ikatumwa kwa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya kupitia mwakilishi wa baba mtakatifu nchini Kenya Apostolic Nuncio Hurbetus Van Megen. Askofu mteule Mwongela anachukua nafasi hii baada ya askofu Antony Muheria aliyehamishwa kwenda kuhudumu katika diosesi ya Nyeri mnamo 23rd Aprili 2017.