Staff Mail

CATHOLIC DIOCESE OF ISIOLO COMMUNICATION DEPARTMENT

MWANARIADHA AKAMATWA KATIKA BURUDANI SAA YA KAFYU

Na Wanjumbe Kamachu.... Mwanariadha matata katika fani ya masafa marefu wilison kipsanga kiprotich,, amejipata pabaya baada ya kutiwa baroni katika kaunti ya elgeyo markwet. Kipsanga na mwenye umri wa miaka 38 amekamatwa na mwakilishi wa wadi wa kapchemutwa ambrose kiplagat wakiwa eneo la burudani wakijivinjari kwa pombe wakati wa masaa ya kafyu. Ikumbukwe kuwa mwanariadha huyu alipigwa marufuku ya kushiriki mbio baada ya kupatikana na makosa ya kutumia dawa za kusisimua misuri Insert…. Kilabu ya kakamega homeboyz imekuwa kilabu ya kwanza nchini kutangaza kupunguza mshahara wa wachezaji kwa asilimia 50 ili kusaidia kupigana na corona na pia kusaidia ligi kuu nchini. Kakamega homeboyz wamekuwa na msimu wa kufana wakiwa nambari mbili jedwalini. ……………………………………………………. Na tukizama ubelgiji niu kwamba,,, ligi kuu ya ubelgiji imetamatishwa na shirikisho la soka sababu kuu ikiwa ni janga la corona. Kufuatia maamuzi haya club brugge wametawazwa mabigwa wa msimu huu baada ya kuongoza jedwali hilo wakiwa na alama 70. ………………………………………………………… Sky sports ya uingereza imeweza kumchagua sadio mane kama mchezaji bora wa msimu huu . sadio mane amewashinda jordan herdeson na kelvin debyune. Mane mzawa wa senegali amekuwa akitambaa vilivyo