Staff Mail

CATHOLIC DIOCESE OF ISIOLO COMMUNICATION DEPARTMENT

SWAALA LA ARDHI KUWA DONDA SUGU ISIOLO

Vijana katika eneo la bula pesa Kaunti ya Isiolo wameomba serikali ya kaunti kuingilia kati katika mgogoro wa ardhi uliozuka jana mchana wakidai kuwa wananyanganywa shamba na wenzao . Vijana hao walishambuliwa na nyumba zao kuteketezwa na kubomolewa walipokuwa wameenda kanisani ila hawajui sababu ya kushambuliwa na waliripoti kisa hicho katika kituo cha polisi. Baadhi wa vijana wameomba serikali kuingilia kati ili kuzuia mgogoro wa ardhi uliopo baina ya vijana . Aidha wameongeza kuwa vijana waliokuja kuwashambulia walikuwa wamebeba silaha wanahofia maisha yao yapo hatarini.Wameomba serikali kuwapa stakabadhi za ardhi hio ili kuzuia mzozano kati yao. Msimamizi wa eneo la Bula kati A wario Elgoi ameomba serikali ya kaunti kuingilia kati ili kuleta amani kuzuia kati ya vijana hao ili kusulisha mgogoro wa ardhi ambao unaeza leta hasara na kuwapoteza vijana. Pia amewaonya vijana wanaotumia silaha kuwa watakamatwa.