Staff Mail

CATHOLIC DIOCESE OF ISIOLO COMMUNICATION DEPARTMENT

TANZANIA YARIPOTI VISA VIWILI ZAIDI VYA MAAMBUKIZI VYA CORONA

Tanzania imeripoti kuongezeka kwa visa viwili zaidi vya maambukizi ya virusi vya corona, huku Shirika la afya duniani likilionya bara la Afrika kujiandaa kwa hali mbaya zaidi ya virusi hivyo. Kuongezeka kwa visa viwili kunaifanya Tanzania kuwa na idadi ya visa vya coronavirus vitano baada ya visa vingine vitatu kutangazwa mapema wiki hii. Mgonjwa wa kwanza alisafiri katika mataifa ya Uswiss, Denmark na Ufaransa kati ya tarehe 5 na 13 Machi na kurejea nchini tarehe 14 Machi 2020. Mwanaume wa pili alisafiri nchini Afrika akusini baina ya tarehe 14 na 16 Machi na kurudi nchini Tanzaniatarehe 17 Machi 2020. Kwamujibu wa Wizara ya afya wanaoume hao wote wawili wametengwa.