Staff Mail

CATHOLIC DIOCESE OF ISIOLO COMMUNICATION DEPARTMENT

WALIOSTAAFU WAOMBA USAIDIZI ISIOLO

Viongozi waliofanya kazi na serikali ya rais moi na ile ya rais kenyatta kutoka kaunti ya isiolo wametoa wito wa serikali kuu kuongeza pesa wanazopata kila mwezi. Wameeleza kwamba wanapokea shilingi elfu nne pekee yake tofauti na wambuge ambao watakuwa wanapokea shilingi elfu mia moja kwa kila mwezi iwapo rais kenyataa atatia saini mswada uliombele yake. Wakizungumza mjini Isiolo wazee hao wameeleza kwamba bado wanaishi kwa umaskini licha ya kufanyia serikali kazi kwa kipindi kirefu. Aidha wamedokeza kwamba wamekuwa wakituma barua kwa ofisi ya rais kenyatta ila wanabaki bila kupata majibu vile vile wamerai uhuru kenyatta kutumia muda uliobaki kwa kuwashughulikia angalau wapate fedha zaidi. NA WANJUMBE KAMACHU