Staff Mail

CATHOLIC DIOCESE OF ISIOLO COMMUNICATION DEPARTMENT

WENYEJI ENEO LA KANGUTO WADI YA BULA PESA WALALAMIKIA SWALA LA MAJI TAKA WANAYODAI KUWAADHIRI KIAFYA

Wakaazi wa Kangutu katika wadi ya Bulapesa wameonyesha kutoridhishwa na jinsi serikali ya kaunti inavyoshughulikia suala la maji taka katika eneo hilo. Wakizungumza na radio Shahidi wakaazi hao wametoa malalamishi yao wakisema kuwa wameathirika kiafya kwa kuwepo kwa mabomba ya maji taka yaliyopasuka katika eneo hilo. Aidha wakaazi hao wamedai kuwa barabara hazipitiki kwa kuharibiwa na maji taka na uvundo kuvuma katika eneo hilo wakidai kuwa wametelekezwa kama wakaazi wa kaunti ya Isiolo. Wametoa wito kwa serikali ya kaunti kuingilia kati na kutafuta suluhu la kudumu kwa kuwatengezea mabomba maji taka yatakayostahimili eneo hilo wakieleza kuwa yaliyoko sasa hivi na yanatishia maisha yao kwa kuwa yako wazi na huenda yakasababisha magonjwa kama vile kipindupindu. NA JACKLINE MUNG'ATHIA